Shirika la kimataifa la Amnesty
International,limetuhumu makampuni makubwa ya mafuta ikiwemo Shell kwa kuficha
ukweli kuhusu kuvuja kwa mafuta nchini Nigeria.
Kwa mujibu wa shirika hilo, makampuni
ya mafuta hudai kuwa mafuta huvuja kutokana na njama za watu wala sio wako
kukosa uadilifu, ili kukwepa kuwalipa fidia waathiriwa.
Amnesty inasema sababu kuu ya
uvujaji, huwa mabomba ovyo au kuu kuu ya makampuni hayo ambayo husababisha
tatizo hilo.
Ripoti ya Amnesty inasema kuwa mpango
wa kufanya usafi baada ya kuvuja mafuta hayo, huwa ina dosari chungu nzima.
Hata hivyo moja ya makampuni
yaliyolaumiwa, Shell, imesema kuwa inakana vikali madai yasiyo na msingi.
Ilielezea tatizo la wizi wa mafuta
ghafi, ambayo ilisema ndio moja ya vyanzo vya uchafuzi wa mazingira katika eneo
la Niger Delta.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos anasema
kuwa kiwango kikubwa cha mafuta yanayovuja yamesababisha uchafuzi mkubwa sana
wa mazingira katika eneo la Niger Delta na uvujaji unafanyika kwa kiwango
kikubwa sana .
Kwa mujibu wa ripoti ya Amnesty,
kulitokea visa 474 vya uvujaji wa mafuta mnamo mwaka 2012 katika eneo moja
pekee, ambalo linamilikiwa na kampuni ya mafuta ya Nigeria Agip Oil.
Ripoti ya Amnesty imetokana na
ushirikiano na mashirika ya kijamii nchini Nigeria kufanya uchunguzi kuhusu
visa vya kuvuja mafuta kwa kipindi cha miezi sita.
Ripoti hiyo imesema kuwa hakuna
ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai ya makampuni hayo kusema kuwa ni wizi na
njama za watu ambazo zimesababisha kuvuja kwa mafuta.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment