Maafisa wawili wa afya nchini Afrika
Kusini wamekamatwa baada ya kuwauzia wagonjwa dawa za kupunguza makali ya
Ukimwi.
Kwa mujibu wa polisi, dawa hizo
hazipaswi kuuzwa bali hutolewa bila malipo kwa waathiriwa wa virusi vya HIV
katika hospitali za umma.
Polisi wa kitengo maalum, walifanya
uchunguzi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wagonjwa.
Wanaume hao watashitakiwa kwa makosa
ya wizi na kupatikana na dawa zinazopaswa kutolewa bure kwa wagonjwa.
"Wagonjwa walilazimika kutoka
hospitalini bila dawa katika hospiali ya Esselen baada ya kuambiwa kuwa hakuna
dawa za ARV. Kisha baadaye walishauriwa na maafisa wawili wa afya waliowaambia
kuwa wanaweza kuwauzia dawa hizo,’’ shirika la habari la Sapa lilimnukuu
msemaji wa kitengo hicho maalum cha polisi, kapteni Paul Ramaloko.
Bwana Ramaloko alisema kuwa washukiwa
walikuwa wanauza dawa hizo kwa dola sita kwa boxi moja ndogo na waliwambia
wagonjwa kuwa dawa hizo zilikuwa zimehifadhiwa kwa wakati wa dharura.
Maafisa hao watafikishwa mahakamani
Ijumaa. Uchunguzi ulianza mnamo mwezi Mei na kukamilishwa Septemba.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg
amesema kuwa ukubwa wa operesheni ya polisi dhidi ya madai hayo haujulikani
wala ukubwa wa kashfa hiyo.
Wanaume hao, walikamatwa Jumatano,
baada ya kuwauzia dawa maafisa wa ujasusi.
"Wale waliokamatwa lazima
wakabiliwe na sheria kwa vitendo vyao," alisema Simon Zwane, msemaji wa
idara ya afya katika mkoa wa Gauteng,’’ liliripoti gazeti la Sapa.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye
idadi, kubwa ya waathiriwa wa virusi vya HIV duniani na maafisa wa afya nchini
humo wanasema kuwa ina mpango mkubwa zaidi wa kutoa dawa za ARV duniani.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment