Gazeti
la Daily Nation la Kenya.
Vyombo vya habari vya Kenya vimekasirishwa na hatua ya bunge
kuupitisha mswaada wa sheria unaoipa serikali nguvu za kuwapiga faini kubwa
waandishi wa habari kwa kwenda kinyume na kile kinachoitwa 'maadili ya
uandishi.'
Katika
mswaada huo uliopitishwa katika kikao kilichokaa usiku sana siku ya Alhamis
(tarehe 31 Oktoba), wabunge wameridhia kuundwa kwa Baraza la Rufaa ya Vyombo
vya Habari na Mawasiliano linaloteuliwa na serikali na ambalo wamelipa uwezo wa
kutoza faini ya hadi shilingi milioni 20 za Kenya (sawa na euro 173,000 ama
dola 234,000 za Kimarekani) kwa wale watakaokutikana na makosa.
Sheria
hiyo pia imelipa Baraza hilo la Rufaa nguvu za hata kumfungia mwandishi wa
habari asifanye kazi zake.
Sheria
hiyo, ambayo sasa inasubiri kusainiwa na Rais Uhuru Kenyatta, inaweka pia
udhibiti mkali kwa matangazo ya redio na televisheni, ambapo vituo hivyo
vinatakiwa kuhakikisha kuwa asilimia 45 ya kile wanachokitangaza kiwe
kimetengenezwa nchini Kenya.
"Sheria
ya ukandamizaji"
Jengo
la Westgate wakati lilipokuwa likishambuliwa mwezi Septemba 2013. Jengo la
Westgate wakati lilipokuwa likishambuliwa mwezi Septemba 2013.
Gazeti
la Daily Nation la Kenya limesema mswaada huo "unaiweka Kenya kwenye
kiwango sawa na Zimbabwe, Cuba, Ethiopia na Kuwait" na kwamba utairudisha
nchi hiyo kwenye "zama za giza".
Gazeti
hilo linaloheshimika nchini Kenya limesema katika tahariri yake ya siku ya
Ijumaa (tarehe 1 Novemba) kwamba "ghafla moja, bunge limezifuta haki za
vyombo vya habari" na kuiita hatua hiyo kuwa ni ya kuogofya ambayo inazua mashaka
kwamba bunge hilo halitashindwa hata kuondoa uhuru wa mahakama hapo baadaye.
Kwa
mujibu wa gazeti la The Star, sheria hiyo mpya ya vyombo vya habari utaipa
serikali "uwezo mkubwa sana" juu ya vyombo hivyo, huku gazeti
jengine, The Standard, limesema sasa demokrasia na uhuru wa maoni nchini Kenya
"vimepigwa dafrau", likiongeza kwamba sheria hiyo ni ya
"ukandamizaji."
Kisingizio
cha usalama wa taifa
Wanajeshi
wa Kenya wakati wa juhudi za kulikomboa jengo la Westgate, Nairobi, mwezi
Septemba 2013. Wanajeshi wa Kenya wakati wa juhudi za kulikomboa jengo la
Westgate, Nairobi, mwezi Septemba 2013.
Kupitishwa
kwa mswaada huo kunakuja wakati kukiwa na mkururo wa kile kinachoitwa
"hatua za kuimarisha usalama wa taifa" kufuatia mashambulizi ya hapo
mwezi Septemba kwenye jengo la maduka la Westgate lililofanywa na wanamgambo wa
al-Shabaab.
Vyombo
vya habari vya Kenya viliingia kwenye mgogoro na mamlaka nchini humo kwa
kutangaza picha zilizochukuliwa kwenye kamera za usalama jengoni humo, ambazo
zinawaonesha wanajeshi wakichukua vitu kutoka baadhi ya maduka na kutoka navyo
nje kwenye mifuko ya plastiki.
Mara
tu baada ya kurushwa kwa picha hizo, mkuu wa polisi, David Kimaiyo, aliwaita
waandishi wawili wa habari na mkuu wa kituo cha televisheni cha KTN kwa ajili
ya kuwahoji.
Kimaiyo
alikuwa amesema kwamba "uhuru wa habari una mipaka yake na kwamba polisi
ilikuwa inawafuatilia kwa karibu waandishi wanaopotosha ambao wangelipandishwa
mahakamani hivi punde.
Baadaye
serikali ilifuta wito huo, baada ya kushambuliwa vikali na vyombo vya habari.
"Baada
ya mashauriano ya kina, wito huo umefutwa," alisema afisa mmoja kutoka
Wizara ya Ndani, akiongeza kwamba waandishi hao wa habari, Mohammed Ali na
Allan Namu wanaoendesha kipindi cha habari za uchunguzi cha Jicho Pevu, na mkuu
wao hawakupaswa tena kuhudhuria kwenye kituo cha polisi kwa mahojiano.
Mwandishi:
Mohammed Khelef/AFP
Mhariri:
Saumu Yusuf
No comments:
Post a Comment