Marekani
imesitisha kwa muda misaada ya kijeshi kwa waasi wa jeshi huru la Syria-FSA.
Kamanda
wa vikosi vya jeshi hilo katika eneo la kusini mwa Syria ambae pia ni
mwakilishi wa waasi katika nchi za magharibi, Abu Ahmed al-Hurani, aliliambia
shirika la habari la Ujerumani- DPA-mjini Amman.
Alisema
alipewa taarifa mapema mwezi Oktoba kwamba Marekani haitawapatia tena misaada
waasi wa FSA, si ya silaha na wala si misaada ya aina yoyote ile nyingine.
Kwa
mujibu wa shirika la habari DW, duru za idara za upelelezi za Marekani katika
mji mkuu wa Jordan, Amman, zimethibitisha taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment