Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo limeanzisha kile wanachokiita "awamu ya mwisho" kuwamaliza
wapiganaji waliobakia wa M23 , baada ya kuichukua ngome ya mwisho katika hatua
ya kuuvunja kabisa uasi huo.
Wanajeshi
wa Kongo wakiwa katika matayarisho ya kufanya mashambulizi 'ya mwisho' dhidi ya
M23.
Mkaazi
mmoja wa mji wa Jomba ulio mpakani mwa Kongo na Uganda, ameliambia shirika la
habari la AFP kwa njia ya simu kwamba sasa "wanajeshi wa Kongo wanaendesha
operesheni zao dhidi ya waasi"kwenye eneo hilo.
Mkaazi
huyo aliyekataa kutaja jina lake amesema amemuona msichana mmoja akiwa
amejeruhiwa kwa risasi katika mapigano ya hivi karibuni kabisa, ingawa
hakufafanua zaidi. "Wanajeshi wa serikali walitumia usiku wao (wa kuamkia
Ijumaa ya tarehe 1 Novemba) hapa na sasa wamekwenda mstari wa mbele wa
mapigano," amesema mtu huyo.
Shirika
la habari la AFP limeripoti kwamba hata wakati wa mazungumzo hayo ya simu,
milio ya risasi ilikuwa inasikikana waziwazi, ambapo chanzo hicho cha habari
kilisema kwamba pande zote mbili za mapigano zilikuwa zikitumia silaha nzito.
Mwandishi wa AFP aliyeko upande wa Uganda aliweza pia kusikia milio hiyo ya
risasi.
MONUSCO
yasaidia
Mkuu
wa MONUSCO, Martin Kobler. Mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler.
Chanzo
kimoja kutoka Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo
(MONUSCO), ambacho kinalisaidia jeshi, amesema mashambulizi hayo dhidi ya M23
ni "awamu ya mwisho," baada ya jeshi hilo kukichukua kituo kikuu cha
waasi cha Bunagana hapo Jumatano.
Lakini
wapiganaji wenye msimamo mkali wa M23, wanaokisiwa kufikia 100, wanasemekana
kujificha kwenye eneo hilo lenye milima mitatu umbali wa kiasi cha kilomita 80
kaskazini mwa mji wa Goma, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini.
"Jeshi
la Kongo limewazunguka wapiganaji hawa wachache wa M23 ili kuwamaliza.
Operesheni inaendelea," kilisema chanzo hicho.
Tangu
mapigano kuanza tena mnamo tarehe 25 Oktoba, baada ya mazungumzo ya amani kuvunjika
nchini Uganda, hakuna wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliojihusisha moja kwa
moja kwenye mashambulizi, lakini MONUSCO imekuwa ikiwasaidia wanajeshi wa
serikali kwa taarifa za kiintelijensia na vifaa.
Kabila
awataka M23 wajisalimishe
Wanajeshi
wa Umoja wa Mataifa katika operesheni za kulinda amani Kongo. Wanajeshi wa
Umoja wa Mataifa katika operesheni za kulinda amani Kongo.
Baada
ya waasi kupoteza makao yao makuu ya Bunagana, siku ya Jumatano Rais Joseph
Kabila aliwasihi tena wapiganaji hao wa M23 kusalimu amri kwa hiyari, akiwaonya
kwamba wakishindwa kufanya hivyo, basi wanajeshi wake wangeliwalazimisha.
Maelfu
ya watu wamekimbia mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa
kundi la M23, ambalo limeundwa na waasi wa zamani wa Kitutsi waliokuwa
wameingizwa kwenye jeshi la Kongo chini ya makubaliano ya amani ya mwaka 2009,
lakini kisha wakaasi mwezi Aprili 2012, wakidai kwamba makubaliano hayo
hayakuwa yametekelezwa kikamilifu.
Mwandishi:
Mohammed Khelef/AFP/Reuters
Mhariri:
Saumu Yusuf
No comments:
Post a Comment