Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, jana ameongoza
mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Luteni Rajab Mlima aliyeuawa Oktoba 27
mwaka huu.
Waombolezaji
wakiwemo askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walionekana
kuwa na huzuni kubwa baada ya mwili huo kuwasili katika Uwanja wa Lugalo 521
KJ.
Akizungumza
baada ya waombolezaji kutoa heshima za mwisho, Bw. Nahodha alisema Luteni Mlima
amekufa wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Alisema
Tanzania haishtushi na mauaji yanayotokea dhidi ya askari wake waliopo nchini
humo wakiwa na jukumu zito la kulinda amani hadi hali itakapotulia.
"Tutaendelea
kupigania amani ya DRC, vifo vinavyotokea dhidi ya askari wetu haviwezi
kuturudisha nyuma," alisema.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samweli
Ndomba, alisema Luteni Mlima aliuawa akiwa katika eneo la mapambano na vikosi
vya waasi wa M23, katika Mlima wa Gavana, karibu na Goma.
Baada
ya mwili wa Luteni Mlima kuwasili Lugalo, ndege mbili za kivita zilipita juu
ili kutoa heshima ya mwisho. Maziko yake yalifanyika jana jioni makaburi ya
Kisutu, Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment