Monday, November 4, 2013

Wakenya wanyakua ushindi wa mbiyo za New York Marathon



Kwa mara ya tatu Wakenya wanaume na wanawake wanyakua ushindi wa mbiyo maarufu ya New York Marathon. Walinyakua taji kwa pamoja ushindi kama huo mwaka 2002 na 2003. Nchi nyingine iliyoweza kufanya hivyo ni Marekani hapo 1977.

Mkenya Priscah Jeptoo alikimbia kwa mara ya kwanza katika mbiyo hizo na kuweza kunyakua ushindi upande wa wanawake kwa kutumia saa 2 dakika 25 na sekunde 7 na kumtupa mbali kwa dakika moja Methopia Buzunesh Deba.

Jeptoo aliyetarajiwa kushinda mbiyo hizo za New York baada ya kunyakua ushindi wa mbiyo za marathon za London atapokea dola laki tano kwa kunyakua pia taji la Mshindi wa Mbiyo za Marathon Duniani.

Mwenzake Geoffery Mutai alishinda mbiyo za anaume akitumia muda wa  saa 2:08:24. Methopia Tsegaye Kebede alichukua nafasi ya pili akiwa karibu dakika moja nyuma ya Mutai na kuchukua taji la Mshindi wa Mbio za Marathon Duniani.
Chanzo: VOASwahili

No comments: