Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Misri Nabil Fahmy
Ikiwa ni ziara yake ya kwanza
kutembelea Misri tangu kung'olewa madarakani kwa Rais Mohammed Morsi, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry ametaka kumalizwa kwa aina zote za ghasia
na kutaka kuwepo maendeleo ya kidemokrasia nchini Misri.
"Historia imeonyesha kuwa
demokrasia inakuwa imara zaidi na kustawi kuliko njia nyingine yoyote
ile," ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Cairo.
"Kwa kuwa na utulivu unakuja
utalii na uwekezaji, kwa vyote viwili, zinakuja fursa za ajira kwa wananchi wa
Misri."
Amesema, Misri ni mshirika
"muhimu" wa Marekani.
Mwezi uliopita Marekani ilisitisha
kubwa ya msaada wa dola bilioni 1.3 za Kimarekani, ambazo nchi hiyo imekuwa
ikiipatia Misri. Misri ilikasirishwa na hatua hiyo ya Marekani.
Bwana Kerry amesema uamuzi huo ni
taswira ya sheria ya Marekani" lakini msaada uliokuwa ukielekezwa moja kwa
moja kwa wananchi, umeendelea kutolewa.
Uhusiano wa mataifa haya mawili
umekuwa wa kihasama tangu kupinduliwa kwa Rais wa Kiislam Mohammed Morsi mwezi
Julai, huku utawala mpya ukifanya msako dhidi ya waandamanaji. Mamia ya watu
wameuawa tangu wakati huo.
Bwana Kerry amesema amekuwa na
mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Misri Nabil Fahmy kuhusu kumalizika kwa
aina zote za ghasia nchini Misri.
"Vitendo vyote vya ugaidi nchini
Misri lazima vikomeshwe- vitendo vyote", amesema.
Bwana Kerry yuko nchini Misri, ikiwa
ni mojawapo ya nchi anazozitembelea katika eneo la Mashariki ya Kati na
kaskazini mwa Afrika.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment