Muungano wa Afrika AU umekosoa baraza
la Usalama la Umoja wa mataifa kwa kupuuza sauti za Waafrika katika maamuzi
yake.
Mkurugenzi wa Baraza la Amani na
Usalama la AU El Ghasim Wane anasema wakati mwingi, baraza la usalama hutoa
maamuzi bila kuzingatia maoni ya Muungano huo.
Wane ameonya kuwa huenda mapendekezo
ya baraza hili yakapuuzwa, iwapo hali itaendelea kama ilivyo.
Wane alikuwa akizungumza kwenye
mkutano uliandaliwa kuangazia suala la ufadhili wa mipango ya usalama na amani
barani Afrika, lakini suala tata la uhusiano wa AU na baraza la Usalama la
umoja wa mataifa, lilijitokeza.
Mkurugenzi wa baraza la amani na
usalama la AU El Ghasim Wane, alisema wakati umefika kwa baraza la usalama la
umoja wa Mataifa kusikiza kwa makini sauti ya Afrika.
Tetesi hizo zinajiri huku baadhi ya
wanachama wa baraza la Usalama la Umoja wa mataifa wakiripotiwa kupuuza ombi la
Umoja wa Afrika la kutaka kesi inayomkabili rais wa Kenya Uhuru Kenyatta,
kusimamishwa kwa muda.
Hata hivyo balozi wa Uingereza katika
AU Greg Dorey alisema suala muhimu kuhakikisha kuwa uhusiano wa Umoja wa
mataifa na AU unaimarishwa.
Huku akitaka muungano huo kuwa katika
mstari wa mbele kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili bara hili.
Walikuwa wakizungumza katika mkutano
wa kujadili jinsi wafadhili wa kimataifa wanavyoweza kuboresha juhudi za AU
kukabiliana na changamoto za kiusalama.
Katika mkutano huo, AU ilikiri kuwa
inaweza kufanya vyema zaidi katika kukabiliana na vita kama vile nchini Mali na
katika Jamhuri ya Afrika ya kati.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment