Spika wa Bunge, Anne Makinda.PICHA|MAKTABA
Na Neville
Meena,Mwananchi
Dodoma.Hoja ya kutaka kumng’oa madarakani
Spika wa Bunge, Anne Makinda imewasilishwa katika Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge, gazeti hili limeelezwa. Hoja hiyo ni ile iliyoanzishwa na
Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla (CCM), ambaye jana aliitisha kikao cha
wabunge wanaomuunga mkono ili kuweka mikakati ya kushinikiza hoja hiyo
iwasilishwe bungeni.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema tayari
wataalamu wake wameifanyia uchambuzi na kwamba, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge
madai ya mbunge huyo tayari yamewasilishwa mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi.
“Tumefanya uchambuzi na ofisi yangu
imeshaipeleka hoja yake katika kamati husika, kwa hiyo sasa mambo yote ni huko
kwenye kamati,” alisema Dk Kashililah.
Wakati hayo yakiendelea, habari
ambazo zilipatikana jana bungeni zinasema, huenda suala hilo likajadiliwa
katika Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM na baadaye kwenye kikao cha wabunge
wote wa chama hicho ili kulipatia mwafaka.
Kulikuwa na taarifa kwamba, Dk
Kigwangalla aliitwa na uongozi wa juu wa wabunge wa CCM kuhusu hoja yake hiyo,
lakini alipoulizwa hakukiri wala kukanusha kuwapo mipango ya chama chake kuteka
hoja yake hiyo.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment