Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Tanzania iko tayari kujitoa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kwani kuna kila dalili ya kutengwa.
Mpasuko wa jumuiya hiyo
umejidhihirisha siku za karibuni baada ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda
kufanya mikutano na kuafikiana kwa mambo kadhaa, huku nchi za Tanzania na
Burundi zikitengwa.
Akijibu maswali ya Wabunge hivi
karibuni Bungeni mjini Dodoma, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta alisema bado Tanzania inatafakari mwenendo huo na inasubiri
mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Jumuiya hiyo wiki mbili zijazo
ili itoe msimamo wake.
Hata hivyo akizungumza na kituo cha
Channel Ten juzi jijini Dar es Salaam, Waziri Membe alisema Tanzania iko tayari
kujitoa na haitapata hasara yoyote.
"Iko wazi tu kwamba
tumeshatengwa na wenzetu...inaweza kuwa sababu pengine tumepeleka majeshi yetu
Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasiamya Congo kuwachakaza, au pengine inawezeka
kuna mtu anataka awe kiongozi (Rais) wa Afrika Mashariki na wengine tukakataa
mpango huo."
"Sisi hatutakubali
kuburuzwa," alisema Membe.
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment