Japan na Urusi zimekubaliana kukuza
ushirikiano kati ya majeshi yao.
Baada ya mazungumzo mjini Tokyo,
waziri wa mambo ya nje wa Japan, Fumio Kishida, amesema hatua hiyo itasaidia
kuimarisha amani na utulivu katika eneo la Asia Mashariki, ambako nchi mbili
hizo zina ushawishi mkubwa.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya
nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amesema ushirikiano wao hautaathiri ushirikiano
uliopo kati ya Japan na Marekani.
Habari zinasema Urusi imekuwa
ikiongeza biashara na mataifa ya Asia na imekuwa ikitafuta uhusiano wa karibu
zaidi na Japan, ikiwa ni kudhibiti kukua kwa ushawishi wa China katika eneo
hilo.
Ijumaa Japan na Urusi zilikubaliana
kuendelea kulitafutia ufumbuzi suala la mgogoro wa mpaka, ambalo limezuia
mataifa hayo kutia saini mkataba wa amani, ambao unamaliza rasmi uhasama wao wa
vita vikuu vya pili vya dunia.
Chanzo: BBCswahili
No comments:
Post a Comment