Mahakama maalumu ya Bangladesh ya
kusikiliza uhalifu wa vitani yametoa hukumu ya kifo kwa Wabangladeshi wawili
walioko uhamishoni, kwa kushiriki kwenye mauaji ya wasomi na waandishi wa
habari 18.
Mauaji hayo yamedaiwa kutokea katika
vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Pakistan mwaka wa 1971, ambavyo vilipelekea
Bangladesh kujitenga na Pakistan.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama
mjini Dhaka kwamba Chowdhury Mueen-Uddin - ambaye sasa anaishi Uingereza - na
Ashrafuzzaman Khan - sasa raia wa Marekani - walikuwa katika kundi la
wanamgambo ambalo likiunga mkono jeshi la Pakistan.
Wanaume hao wawili walifanyiwa kesi
bila ya kuwepo na wamekanusha mashtaka hayo.
Serikali iliwapatia mawakili
kuwatetea ingawa hakuna shahidi aliyeitwa kwa upande wao.
Chanzo:
BBCSwahili
No comments:
Post a Comment