Edward Snowden mfanyakazi wa zamani wa NSA.
Ujerumani na Brazil zimesambaza rasimu ya azimio kwa kamati
ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Ijumaa(01.11.2013) lenye kutowa wito wa
kukomeshwa kwa upelelezi mkubwa wa udukuzi wa mawasiliano kwa njia ya
elektroniki.
Rasimu
ya azimio hilo ambalo nchi zote mbili za Ujerumani na Brazil imelitangaza
hadharani halizitaji nchi kwa majina juu ya kwamba wanadiplomasia wa Umoja wa
Mataifa wamesema ni wazi kuwa lilikuwa limeikusudia Marekani ambayo
imeadhirishwa kutokana na kufichuliwa kwa mpango wake mkubwa wa upelelezi wa
kimataifa na mfanyakazi wa zamani wa shirika la usalama wa taifa nchini humo.
Rasimu
ya azimio hilo la Ujerumani na Brazil italitaka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
lenye nchi wanachama 193 litangaze kwamba "lina wasi wasi mkubwa juu ya
ukiukaji wa haki za binaadamu na dhuluma nyengine ambazo yumkini zikasababishwa
kutokana na upelelezi wa aina yoyote ile wa mawasiliano ukiwemo ule wa
kupindukia mipaka ya nchi."
Pia
linatoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuchukuwa hatua za
kukomesha ukiukaji wa haki hizo na kuweka mazingira ya kuzuwia ukiukaji wa aina
hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba sheria za kitaifa zilizopo wajibu
wake unafuatwa kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya haki za binaadamu."
Yumkini
likahitaji mabadiliko
Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa likiwa katika moja ya vikao vyake mjini New York
Marekani. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likiwa katika moja ya vikao vyake
mjini New York Marekani.
Yumkini
azimio hilo likafanyiwa mabadiliko wakati litakapojadiliwa na Kamati ya tatu ya
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo inalenga suala la haki za binaadamu.
Linatazamiwa kupigiwa kura na kamati hiyo baadaye mwezi huu na badaaye kupigiwa
tena kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi ujao.
Afisa
wa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amekaririwa akisema "
Tumepokea rasimu ya azimio hilo na tutachambua maudhui yake kwa kuzingatia
vigezo vyake."Wanadiplomasia kadhaa wamesema watashangaa iwapo azimio hilo
halitoungwa mkono kwa kauli moja na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Kansela
wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Brazil Dilma Rousseff wote wawili
wamelaani udukuzi uliozagaa uliofanywa na Shirika la Usalama wa Taifa la
Marekani NSA.Madai kwamba NSA imedukiza mawasiliano ya maelfu ya simu za
Wafaransa na kusikiliza simu ya mkono ya Merkel yamechemsha ghadhabu barani
Ulaya.
Azimio
lina uzito gani ?
Hivi
ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa maandamano ya kupinga upelelezi wa NSA
yaliofanyika Washington (26.10.2013). Hivi ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa
maandamano ya kupinga upelelezi wa NSA yaliofanyika Washington (26.10.2013).
Maazimio
ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa kawaida utekelezaji wake unakuwa
haushurutishi kisheria tofauti na maazimio yanayotolewa na Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa lenye nchi wanachama 15.
Lakini
maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambayo yanapata uungaji mkono mkubwa
wa kimataifa yanakuwa na uzito wa kiuadilifu na kisiasa.Azimio hilo litazitaka
nchi kuanzisha taratibu za usimamizi wa kitaifa zenye uwezo wa kuhakikisha kunakuwepo
uwazi na uwajibikaji kwa upelelezi wa mawasiliano unaofanywa na
serikali,udukuzi wao na ukusanyaji wa data za watu binafsi.
Pia
litatowa wito kwa Mkuu wa masuala ya haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Navi
Pillay kuandaa na kuchapisha ripoti kuhusu "ulindaji wa haki ya kuwa na
faragha kwa zingatio la upelelezi wa ndani ya nchi na ule wa kuvuka mipaka ya
nchi ikiwa ni pamoja na upelelezi wa kiwango kikubwa sana, upelelezi wa
mawasiliano, udukuzi wao na ukusanyaji wa data za watu binafsi.
Edward
Snowden mfanyakazi wa zamani wa NSA. Edward Snowden mfanyakazi wa zamani wa
NSA.
Mpango
mkubwa sana wa upelelezi wa Marekani umefichuliwa kutokana na nyaraka
zilizovujishwa kwa vyombo vya habari na mfanyakazi wa zamani wa shirika la NSA
Edward Snowden.Marekani imesema haichunguzi mawasiliano ya Merkel na haitofanya
hivyo kipindi cha usoni lakini haikuzungumzia iwapo iliwahi kufanya hivyo huko
nyuma.
Mapema
wiki hii, Umoja wa Mataifa umesema Marekani imeahidi kutoyafanyia upelelezi
mawasiliano ya Umoja wa Mataifa baada ya kuripotiwa kwamba Shirika la Usalama
wa Taifa la Marekani NSA lilikuwa likidukiza mfumo wa mkutano wa Umoja wa
Mataifa unaofanyika kwa njia ya video.
Mwandishi
: Mohamed Dahman/Reuters
Mhariri:Caro
Robi
No comments:
Post a Comment