Wakuu wa Kenya wameahidi kuchukua
hatua za haraka baada ya watu wa sehemu mbalimbali za dunia kuonesha hasira juu
ya ubakaji wa kikatili aliofanyiwa msichana wa miaka 16.
Inadaiwa kuwa wanaume sita
walimnajisi msichana huyo ambaye alipoteza fahamu, na kisha kumtupa kwenye
lindi.
Watatu kati ya waliokamatwa walipewa
adhabu ya kukata majani tu nje ya kituo cha polisi.
Jaji mkuu wa Kenya, Willy Mutunga,
alisema ameipeleka kesi hiyo mbele ya shirika linalosimamia polisi na mahakama,
National Council for the Administration of Justice, NCAJ.
Watu zaidi ya milioni wametia saini
malalamiko kwenye mtandao kudai haki katika kisa hicho.
No comments:
Post a Comment