Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amewataka
watendaji wa chama hicho nchi nzima, kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa 2014, Uchaguzi Mkuu 2015.
Bw.
Mbowe aliyasema hayo Mjini Kahama, mkoani Shinyanga, mwishoni mwa wiki akiwa
katika ziara ya kichama Kanda ya Ziwa Mashariki, inayojumuisha Mikoa ya Mara,
Simiyu na Shinyanga.
Ziara
hiyo imeanza Novemba Mosi mwaka huu, ambapo Bw. Mbowe alikutana na Baraza la
Mashauriano la mkoani humo na kukagua uhai wa chama katika kanda hiyo.
Pia
Bw. Mbowe alikutana na wadau wa CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki na kupanga
mikakati ya kuimarisha kanda hiyo.
Novemba
2 mwaka huu, alikutana na Baraza la Mashauriano mkoani Mara na kuwataka viongozi
pamoja na wanachama wa Mkoa huo, kuweka mikakati ya kuimarisha hadhi ya chama
ili kufanikisha harakati za ukombozi wa nchi na kupigania mabadiliko kama
inavyokuwa siku zote.
Ofisa
Mwandamizi wa Habari CHADEMA Makao Makuu, Bw. Tumaini Makene, alisema kwa kauli
moja, viongozi wa Baraza la Mashauriano Mkoa wa Mara, waliazimia kuanza
'Operesheni Imarisha CHADEMA Mara', ambayo itazinduliwa hivi karibuni na
kufanyika Mkoa mzima.
Alisema
kupitia uongozi wa kanda wenye mamlaka ya kusimamia na kuimarisha chama katika
mikoa yote husika, Bw. Mbowe amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali kila mmoja
kwa nafasi yake kutimiza wajibu wa kukifanya CHADEMA kiendeleekuwa sauti ya
Watanzania wote, wanaosaka haki nchini.
Aliwataka
wawe viongozi kwa maneno na vitendo akisisitiza umuhimu wao wa kuwa taswira
chanya mbele ya jamii pamoja na kukiwakilisha chama kwa kuzingatia uadilifu,
uwezo na uwajibikaji kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania ambao chama hicho
kinataka kuwaongoza.
Bw.
Mbowe alisisitiza umuhimu wa vikao vya kikatiba, mafunzo na mikutano ya
wanachama katika usimamizi, uendeshaji wa chama hasa wakati huu ambao
Watanzania wameweka matumaini ya kufanya mabadiliko ya kimfumo na kiutawala,
kupitia CHADEMA
Chanzo:
Majira
No comments:
Post a Comment