Waathirika wa kesi inayomkabili rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa kutaka
kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya kimataifa ya
ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika
wameandaa rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe
kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la kigaidi
katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.
Lakini mwanasheria wa waathirika,
Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya kupatikana
haki kwa waathirika. Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka yanayomkabili dhidi ya
uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007
Chanzo:BBCSwahili
No comments:
Post a Comment