Dar es Salaam na Mikoani.Mtihani wa kidato cha nne ulioanza
jana nchini, umeingia dosari baada Omary Mkumbo (25) Mkazi wa Mwangata C,
Manispaa ya Iringa, kufariki dunia kwa kujinyonga akihofia kufeli mtihani.
Mkumbo alitarajia kuanza mtihani jana
kwenye Kituo cha The dream Centre kilichopo Kata ya Gangilonga, mkoani Iringa.
Hata hivyo, alikutwa amejinyonga huku
akiacha ujumbe chumbani kwake usiku wa kuamkia jana unaosomeka: “Buriani,
nimechoka kufeli mtihani”.
Shangazi wa marehemu, Betha Nzogu
(60) alisema Mkumbo alitarajia kuanza mtihani jana ikiwa mara ya tatu tangu
alipohitimu kidato cha nne mwaka juzi na kufeli, kisha tukio kama hilo
kujirudia mwaka jana.
Alisema kabla ya kuchukua hatua hiyo,
Mkumbo alimsaidia kuchinja kuku ambazo huziuza na kwamba, baada ya kumaliza
kazi hiyo alirudi nyumbani kwake na kuanza kazi ya kufua nguo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Mwangata C, Saleh Mgimwa alisema alipata taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo
saa 3:30 usiku.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa,
Ramadhan Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na chanzo ni hofu ya kufeli
mtihani.
Wakati hayo yakitokea, Dar es Salaam
mwanafunzi Asmah Furahisha wa Sekondari ya Kenton iliyoko Sinza, alishindwa
kuungana na wenzake baada ya kuzimia dakika chache baada ya kuitwa kuanza
mtihani wa jiografia.
No comments:
Post a Comment