Aliyekuwa kiongozi wa Palestina
Yasser Arafat huenda aliuawa kwa sumu kali ya Polinium.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya
kisayansi iliyofanywa na wanasayansi nchini Uswizi ambayo shirika la bahari la
Al Jazeera limeweza kupata.
Hata hivyo ripoti za awali kulingana
na rekodi za kimatatibu zake hayati Arafat zinasema kuwa alifariki kutokana na
kiharusi , kilichosababishwa na ugonjwa wa damu.
Lakini mwili wake ulifukuliwa mwaka
jana kwa uchunguzi zaidi kutokana na madai kuwa Arafat aliuawa.
Ripoti hiyo ya wanasayansi kutoka
Uswizi, inasema kuwa mwili wa Arafat ulionyesha dalili za kuwa na kiwango
kikubwa cha sumu ya Polonium, na hivyo kuunga mkono dhana ya kuuawa kwake kwa
sumu.
Wapelestina wengi wameamini kwa miaka
mingi kuwa Israel ndio ilimuua Aarafat kwa sumu. Wengine wanadai kuwa alifariki
kutokana na ugonjwa wa Ukimwi au Saratani.
Israel imekuwa ikikana madai ya
kuhusika na mauaji ya hayati Arafat.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa
Israel, amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa Uswizi ni kama
mchezo wa kuigiza tu.
Wanasayansi hao walifanyia uchunguzi
wa kina nyaraka za kimatibabu za Arafat, wakachunguza mabakai yake pamoja na
vitu alivyokwenda navyo hospitalini mjini Paris kutafuta matibabu alipofariki
mwaka 2004.
Walifanyia uchunguzi mifupa yake
pamoja na mchanga katika sehemu alikozikwa Arafat.
Wanasayansi hao walisema kuwa matokeo
ya utafiti wao yanawiana na madai ya Arafat kuuawa kwa sumu aina ya
Polonium-210.
Chanzo:
BCSwahili
No comments:
Post a Comment