Kesi
dhidi ya aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi imeahirishwa muda mfupi baada
ya Morsi kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuchochea mauaji.
Morsi
alimwambia jaji kuwa mashitaka dhidi yake sio halali kwani yeye angali rais wa
Misri na ambaye alichaguliwa kwa njia ya demokrasia.
Baada
ya matamshi ya Morsi, yalisababisha jaji kuahirisha kesi dhidi yake na kusema
kuwa itasikilizwa tarehe nane mwezi Januari.
Wanachama
wengine 14 wa ngazi za juu wa kundi la Muslim Brotherhood pia wameshitakiwa na
mashitaka kama hayo.
Kesi
hiyo inafanyika katika kituo cha mafunzo ya polisi ambapo kuna ulinzi mkali.
Vyombo
vya habari vya kitaifa vimeripoti kwamba jaji wa kesi hiyo alilazimika
kusitisha kwa mda kesi baada ya washtakiwa kuimba huku bwana Mosri akikataa
kuvaa vazi la mahakamani akidai kuwa yeye nidye rais halali.
Mohammed
Morsi alifikishwa katika chuo hicho kwa ndege aina ya helikopta kutoka eneo la
siri ikiwa ndio mara yake ya kwanza kuwahi kuonekana hadharani tangu aondolewe
mamlakani mwezi Julai mwaka huu.
Makundi
ya waandamanaji tayari yamekusanyika nje ya chuo hicho cha mafunzo ya polisi
huku wengine wakiimba nyimbo za kupinga jeshi la taifa hilo.
Maafisa
wa kijeshi katika taifa hilo wanaendelea kushika doria katika mji wa Cairo na
miji mingine baada ya wafuasi wa Bwana Morsi kuitisha maandamano makubwa.
Morsi
aliondolewa uongozini kwa nguvu za jeshi mwezi Julai baada ya maandamano ya
kila mara kufanyika kupinga utawala wake.
Ingawa
alishinda urais kwa njia ya demokrasia, wakati wa uongozi wake wa zaidi ya
mwaka mmoja, Morsi hakuelewana sana na taasisi nyingi za serikali.
Polisi
na jeshi wamedhibiti hali ya usalama kote Misri
Baada
ya kupinduliwa na jeshi, maandamano yalifanyika kila kulipokucha mjini Cairo na
makubwa zaidi yalikuwa ya wafuasi wake kukesha karibu na kasri la rais wakitaka
Morsi aachiliwe.
Polisi
walaisababisha mamia ya vifo vya wafuasi hao walipovunja maandamano yao kwa
nguvu.
Serikali
ya muda pia imekuwa ikiwasawa na kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood,
chama chake Morsi.
Serikali
pia imeharamisha vyama vyote vya kisiasa huku ikiwakamata mamia ya viongozi wa
mashirika hayo.
Wafuasi
wake wanasema kuwa alipinduliwa na jeshi na sasa anakabiliwa na kesi ya
kisiasa.
Mashirika
ya kutetea haki za binadamu, yameituhumu maafisa wa usalama kwa kufanya kazi
yao bila uwajibikaji.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment