Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama
hicho imepokea barua iliyoandikwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Zitto Kabwe.
Barua
hiyo, inamtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Wilbrod Slaa athibitishe madai
ya ripoti inayosema“Taarifa ya Siri ya CHADEMA”iliyosambazwa katika mitandao
mba limbali ya kijamii.
Taarifa
hiyo inadai kuchunguza mwenendo wa Bw.Kabwe tangu mwaka 2008-2010 na kubaini
amepokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuivuruga CHADEMA.
Akizungumza
na Majira jana, Ofisa Habari wa CHADEMA,Tumaini Makene,alise ma barua
aliyoiandika Bw. Kabwe itafanyiwa kazi kwa mu jibu wa taratibu, kanuni za
katiba ya chama.
“Chama
chetu kinaongozwa na vikao hivyo barua yake itafanyiwa kazi...CHADEMA h
aiendeshwi na taarifa za magazetin i au mitandaoni,”alisema Bw. Makene.
Aliongeza
kuwa,si mara ya kwanza makundi yasiyojulikana kusambaza taar ifa za kutaka
kumchafua Bw. Kabwe k upitia mitandao hiyo ambapo Ofisi ya
Habari,ilishughulikia suala hil o na kuhakikisha taarifa hizo zinaondolewa.
“Hivi
sasa ni mara ya pili, Bw. Kabwe anali fahamu hilo hivyo CHADEMA hakihusiki,
lakini kitashughulikia suala hili kupitia vikao ili kupata majibu sahihi,”
alisisitiza Bw.Makene.
Katika
taarifa yake aliyoitoa juzi kwa vyombo vya habari, Bw.Kabwe alisema taar ifa
hizo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii hiv yo alimtaka Dkt.Slaa,
athibitishe kinachoitwa“Ta arifa ya Siri ya CHADEMA”,kama ni taa rifa ya chama
au kiikanushe ili kumpa fursa ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi
wa taarifa hiyo.
Hata
hivyo, Bw. Kabwe ambaye pia ni Mbunge w a Kigoma Kaskazini,aliziita taarifa
hizo za kutunga zilizojaa uongo wa kiwango cha kutisha hali ambayo
imemfedhehesha, kumsikitisha na kumkasirisha.
Alisema
taarifa hizo ziliibuliwa katika kipindi am bacho alikuwa safarini kutetea haki
za Watanza nia na Afrika ambao utajiri wao wa rasilimal i unafaidiwa na watu
wachache waliohifadhi fedha katika akaunti nje ya nchi.
Chanzo:
Majira
No comments:
Post a Comment