Misri inasemekana kuwa nchi yenye rekodi mbaya zaidi ya haki
za wanawake katika mataifa ya kiarabu. Hii ni kwa mujibu wa kura ya maoni
iliyofanywa na wataalamu wa maswala ya kijinsia.
Utafiti huo uligundua kuwa wanawake wanadhulumiwa sana
kingono, visa vingi vya ukeketaji wa wasichana na ongezeko la makundi ya watu
wenye itikadi kali kuwa baadhi ya mambo yanayochangia dhuluma dhidi ya
wanawake.
Visiwa vya Comoros vilishikilia nafasi ya kwanza katika
utafiti huo uliofanywa na wakfu wa Thomson Reuters.
Zaidi ya wataalamu 330 wa maswala ya jinsia walihojiwa
katika nchi 21 za kiarabu ikiwemo Syria.
Huu ni utafiti wa tatu wa aina hii kufanywa na wakfu huo
uliolenga hasa haki za wanawake tangu harakati za mapinduzi kuanza kushuhudiwa
katika nchi za kiarabu mwaka 2011.
'unyanyasaji kila siku'
Iraq ilishikilia nafasi ya pili baada ya Misri ikifuatiwa na
Saudi Arabia, Syria na Yemen kuwa miongoni mwa nchi zenye rekodi mbovu kuhusu
haki za wanawake.
Nchini Comoros ambako wanawake wanashikilia asilimia 20 ya
nyadhifa za mawaziri, inafuatiwa na Oman, Kuwait, Jordan na Qatar.
Kura ya maoni iliwataka wataalamu kutathmini maswala kama
dhulumua dhidi ya wanawake, haki za afya ya uzazi , ambavyo wanawake
wanatendewa katika familia na jukumu la wanawake katika siasa na uchumi.
Sheria zinazochochea ubaguzi dhidi ya wanawake pamoja na
biashara haramu ya binadamu ndizo sababu zilizochangia Misri kuwa na rekodi
mbaya zaidi katika ambavyo wanawake wanatendewa katika nchi 22 za kiarabu.
Nchini Misri kuna sehemu ambazo shughuli za kiuchumi na
biashara zinazingatia sana biashara haramu ya kuwauza wanawake na kuwafanyisha
ndoa za lazima.
Hata hivyo dhuluma za kingono ndio changamoto kubwa zaidi
dhidi ya wanawake.
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Aprili
ilisema kuwa asilimia 99.3 ya wanawake wamedhulumiwa kingono.
Wakati huo huo, Iraq imesemekana kuwa mahala hatari sana kwa
wanawake kuishi kuliko ilivyokuwa chini ya utawala wa hayati Saddam Hussein..
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment