Waziri
Mkuu mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Frederick Sumaye, leo anatarajia kuzungumza
na waandishi wa habari pamoja na kutoa tamko la kumuunga mkono Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Rais Jakaya Kikwete kwa kauli yake ya kukemea rushwa
ndani ya chama hicho hasa kwa watu wanaotafuta madaraka.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu kinasema kuwa, Bw. Sumaye atatoa tamko hilo leo saa tatu
asubuhi katika Hoteli ya Court Yard iliyopo Upanga, Dar es Salaam.
Chanzo
hicho kiliongeza kuwa, pamoja na kuto a tamko hilo pia atazungumzia tukio la
hivi karibuni akidaiwa kuhujumiwa mwaliko aliopewa na vijana wa asasi ya
kuelimisha jamii kuhusu usalama na amani (Public Ter rorism Awareness Trust
Fund and Human Welfare(PTA-HW).
Asasi
hiyo iliandaa tamasha ambalo lilipa ngwa kufanyika katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja,Dar es Salaam na kumwalika Bw. Sumaye kuwa mgeni rasmi lakini katika
mazingira ya kutatanisha , saa chache kabla ya shu ghuli hiyo aliambiwa
imeahirishwa na atataarifiwa tarehe nyingine itakayopangwa.
Katika
hali isiyo ya kawaida, maandamano ya vij ana hao yaliwasili katika viwanja
hivyo ambapo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kutoka Wilaya ya Bukoba
Vijijini, mkoani Kagera, Bw. Naziri Karamagi, aliyapokea maandamano hayo.
Dalili
za mgawanyiko miongoni mwa waandaaji,zilijitokeza baadaya kuwasili kwa
Bw.Karamagi ambaye hakuwa ametarajiwa na waandaaji pamoja na washiriki wa
tamasha hilo.
Baadhi
ya vijana walioshiriki tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na vikundi 41 vya
vijan a kutoka Da res Salaam, Zanzibar na Pwani, wa lisikika wakilaumu
mabadiliko ya mgeni rasmi.
Chanzo:
Majira
No comments:
Post a Comment