Wawakilishi wa tume ya nishati kutoka
vyama ndugu vya Christian Democratic CDU na Social Democratic SPD wazungumzia
mageuzi katika sekta ya nishati
Waziri
wa mazingira Peter Altmeier wa chama cha CDU na waziri mkuu wa jimbo la
Northrhine Westfalia,bibi Hannelore Kraft wa chama cha SPD
Matumizi
ya nishati mbadala nchini Ujerumani ndio yaliyogubika mazungumzo ya kuunda
serikali kuu ya muungano mjini Berlin.Mada kuu ni kuhusu namna ya kupunguza
kupanda bei ya nishati wakati Ujerumani inajiandaa kuondokana na nishati ya makaa
mawe na kuingia katika enzi za nishati inayotokana na nguvu za upepo na
mwangaza wa jua.
Waziri
mkuu wa jimbo lenye wakaazi wengi zaidi la Ujerumani-Northrhine Westfalia,bibi
Hannelore Kraft wa kutoka chama cha Social Democratic-SPD pamoja na waziri wa
nishati wa serikali kuu inayomaliza wadhifa wake Peter Altmeier wa chama cha
Christian Democratic Union CDU ndio wanaoongoza mazungumzo ya tume
inayaoshughulikia mageuzi katika sekta ya nishati.
Alipoteremka
ndani ya gari tu bibi Hannelore Kraft alitambua nini kinamsubiri.Wanaharakati
wa shirika la usafi wa mazingira Green Peace wamekusanyika mbele ya wizara ya
mazingira katika uwanja wa Postdam na magari matano yaliyojaa makaa mawe na
karibu na hapo sampuli za mitambo ya nishati ya upepo."Nishati mbadala
badala ya kugharimiwa makaa mawe" ndio ujumbe wa wanaharakati hao kwa
waziri mkuu huyo wa jimbo la Northrhine Westfalia.
Nishati
mbadala inayotokana na nguvu za upepo-mradi unaoendeshwa katika jimbo la
Schleswig-Holstein
Sheria
ya mageuzi kufanya kazi mwaka 2015
Saa
sita nzima walihitaji wajumbe wa tume ya mazungumzo kujadiliana kuhusu nishati
mnamo duru hiyo ya kwanza .Magharibi ilipoingia matokeo yakatangazwa:Vyama
ndugu vya CDU na CSU vinavyoongozwa na kansela Angela Merkel na kile cha Social
Democratic vinataka mswaada wa sheria mpya ya mageuzi ya nishati ifikiwe hadi
msimu wa kiangazi mwakani .Bunge la shirikisho Bundestag na baraza la
wawakilishi wa majimbo Bundesrat,yakiidhinisha mswaada huo ,sheria ya mageuzi
ya nishati ianze kufanya kazi mapema mwaka 2015.
Pande
zote mbili zinaonyesha kuridhika na maridhiano yaliyofikiwa katika duru hiyo ya
kwanza ya mazungumzo.Waziri mkuu wa jimbo ambalo kijadi ndio shina la migodi ya
makaa mawe,bibi Hannelore Kraft amekanusha tuhuma kwamba anayapigania mashirika
ya makaa mawe .Waziri wa mazingira Peter Altmaier anayataja mageuzi ya sekta ya
nishati kuwa "mradi mkubwa zaidi wa serikali kuu ya muungano."Anasema
"Ujerumani inabidi iutanabahishe ulimwengu kwamba nishati mbadala inaweza
kupatikana kwa bei nafuu".
Hapo
waziri wa nishati alikuwa akijibu hoja kwamba licha ya kuporomoka bei jumla ya
umeme,majumbani watu wanalipa bei kubwa kabisa kufidia nishati mbadala.
Mgodi
wa makaa mawe huko Garzweiler katika jimbo la Northrhine Westfalia
Kipindi
cha mpito kipite salama
Waziri
mkuu Hannelore Kraft,anaeshirikiana serikalini na walinzi wa mazingira die
Grüne mjini Dusseldorf amekanusha tuhuma kwamba anayapigania mashirika ya makaa
mawe."Tunataka kipindi cha mpito kuelekea nishati mbadala kifanyike
salama,watu wamudu na kiambatane na usafi wa mazingira" amesema.
Mkuu
wa chama cha walinzi wa mazingira Simone Peter aliwaonya CDU/CSU na SPD dhidi
ya kile alichokiita kurejea nyuma na kutoa ruzuku kwa migodi isiyokuwa na tija
ya makaa ya mawe.
Duru
ya pili ya mazungumzo ya tume inayoshughulikia masuala ya nishati itaendelea
jumatatu ijayo mjini Berlin.
Mwandishi:Hamidou
Oummilkheir/dpa/AFP
Mhariri:Yusuf
Saumu
No comments:
Post a Comment