Zanzibar.Wakati wabunge wakitaka posho ya
vikao iongozwe kutoka Sh100,000 hadi Sh300,000 kwa siku, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ) imepandisha posho kutoka Sh100,000 hadi 150,000 kuanzia mwaka
huu.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini
viwango hivyo vya posho vimeanza kutumika tangu kupitishwa kwa bajeti ya mwaka
2013/14, kila mjumbe analipwa kiwango hicho cha posho licha ya mshahara wake.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar (BLW), Yahya Khamis Hamad alithibitisha viwango hivyo vipya vya posho
kuanza kutumia mbali na mishahara yao na posho mbalimbali za jimbo kila mwezi.
Hamad alisema nyongeza hiyo ya kikao
imetokana na mapendekezo ya Kamati ya Uongozi ya BLW, baadaye kuridhiwa na Rais
wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Alisema kutokana na kupanda kwa
gharama za maisha, kamati ya uongozi ina wajibu wa kuangalia kila mwaka maslahi
ya wawakilishi, lakini mwaka jana posho za vikao hazikuangaliwa badala yake
ziliangaliwa posho nyingine na mishahara yao.
Mabadiliko ya posho ya vikao mishara
na posho mbalimbali za wajumbe yalifanyika mwaka 2012/13, kutoka Sh3.5 milioni hadi
Sh4.5 milioni.
Chanzo:
Mwananchi
No comments:
Post a Comment