Muundo wa Matokeo ya sasa Picha ya pili na kwa sasa picha ya kwanza
Serikali
imefanya marekebisho ya upangaji wa viwango vya alama kwa wanafunzi wa kidato
cha nne, sita pamoja na matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi kwa ajili ya
kuamua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.
Marekebisho
hayo yametokana na maoni ya wadau wa elimu ambapo kwa muda mrefu sasa, upangaji
viwango vya alama vinavyotumika katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na
sita, haufanani wakati mitihani yote ni ya sekondari.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, aliyasema
hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua
kuwa, muundo huo utatumika kwa miaka minne.
"Utatumika
kwa miaka minne kabla haujahuishwa ili kuupa muda wa kutosha kuona aina ya
changamoto zinazojitokeza na jinsi ya kuzishughulikia," alisema Prof.
Mchome.
Marekebisho
hayo ni utekelezwaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa katika sekta hiyo (Big
Results Now), ambapo daraja sifuri, limefutwa na kuwekwa daraja ambalo
litafahamika kama daraja la tano.
"Daraja
la tano ndio la mwisho kabisa katika ufaulu, mabadiliko haya yatapunguza idadi ya
wanafunzi wa wanaofeli kuanzia 2013 (kidato cha nne) na kidato cha sita 2014.
"Kuanzia
sasa, daraja la kwanza I, litaanzia pointi 7-17, II (18-24), III (25-31), IV
(32-47) na daraja la V (48-49)," alisema.
Awali,
katika muundo wa zamani, daraja la I lilianzia pointi 7-17, ambayo
haijabadilishwa, II (18-21), III (22-25), IV (26-33) na daraja sifuli lilianzia
pointi 34-35.
Alifafanua
kuwa, daraja la kwanza ni kundi la ufaulu ambao umejipambanua na bora sana, II
ufaulu mzuri sana, III ufaulu mzuri na wastani, IV ufaulu hafifu na V ufaulu
usioridhisha.
Aliongeza
kuwa , alama endelevu mwaka 2013 kwa wanafunzi wa kidato cha nne, tayari
zimewasilishwa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), ambapo alama hizo zichangie
asilimia 40 katika mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.
Prof
. Mchome alisema , wataalamu wa mifumo ya mitihani, watalifanyia kazi zaidi
suala la madaraja liweze kutumika kwa ufanisi katika kipindi hiki cha mpito.
"Mabadiliko
hayo yamefanyika ili kuendelea kuimarisha mfumo wa elimu, kuweka wazi taratibu
mbalimbali kwa ajili ya mitihani na masuala mengine.
"Sera
ya elimu na mafunzo ya 1995 imeelekeza kwamba, katika kuamua kiwango cha ufaulu
wa mwanafunzi wa sekondari, alama za tathmini endelevu ya mwanafunzi zitachangia
asilimia 50 na mtihani wa mwisho asilimia 50.
"Upande
wa Zanzibar, alama hizi zimekuwa zikiandaliwa kwa mfumo wa asilimia 40 na
mtihani wa mwisho asilimia 60," alisema na kuongeza kuwa, wadau wengi
walishauri muundo uliopo sasa wa madaraja, uimarishwe na kuanza kutumia muundo
wa wastani wa alama katika ufaulu (GPA) ambao ni rahisi kueleweka.
Alisema
matumizi ya muundo wa GPA ni rahisi kukadiria uwezo wa mwanafunzi kielimu na
kufanya maamuzi yakiwemo ya kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali za
elimu.
"Kutokana
na idadi kubwa ya wanafunzi walio katika mfumo wa elimu wapo katika ufaulu
hafifu, Serikali imeona kuna mambo mengi ambayo hayana budi kuendelea
kuimarishwa," alisema.
Mambo
hayo ni pamoja na mfumo wa mitaala, walimu, mazingira ya kujifunzia,
kufundishia, vitabu na vifaa vingine muhimu.
Katika
hatua nyingine, Wizara hiyo imesema mtihani wa kidato cha nne na mtihani wa
maarifa mwaka huu, unatarajiwa kufanyika nchini kote kwa siku 18 kuanzia
Novemba 4 hadi 21.
Prof.
Mchome alisema watahiniwa walioandikishwa kufanya mtihani huo ni 427,906 kati
yao 367,399 wa shule 60,507 watahiniwa wa kujitegemea.
Aliwataka
walimu, wasimamizi wa mitihani, wakuu wa shule, viongozi na jamii kuhakikisha
mitihani inafanyika katika hali ya amani, utulivu na asitokee mtu akajaribu
kuharibu taratibu kwani ni kosa la jinai na atachukuliwa hatua.
"Uharibifu
wa taratibu hauna faida katika jamii kwani mitihani ya kidato cha nne ni muhimu
katika Taifa kwa maendeleo ya jamii na sekta ya elimu.
"Natoa
wito kwa kamati za mitihani mikoa yote, kuhakikisha taratibu zote za utunzaji,
uhifadhi na usafirishaji wa mitihani zinazingatiwa," alisema.
Alisema
hadi sasa maandalizi na usafirishaji mitihani hiyo ngazi ya Mkoa, yamekamilika
pamoja na usalama wa mitihani ambapo hakuna uliovuja katika ngazi yoyote
kuanzia NECTA, mikoa na halmashauri
Chanzo:
Majira
No comments:
Post a Comment