Saturday, November 2, 2013

Wanasheria Kenya wamtaka Kenyatta kupinga mswada wa vyombo vya habari


Chama cha Wanasheria Kenya, LSK kinasema kinatayarisha pendekezo la kumkabidhi Rais Uhuru Kenyatta ili asitiyesaini mswada mpya kuwa sheria, juu ya jinsi vyombo vya habari vinabidi kutangaza nchini humo.

Bunge la Kenya lilipitisha Alhamisi jioni mswada unaounda mamlaka maalum kusimamia vyombo vya habari na kuwataka waandishi habari na vyombo vya habari kujiandikisha na mamlaka hiyo.
Akizungumza na Sauti ya Amerika Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Law Society, LSK Apollo Mboya anasema mamlaka hiyo itakuwa pia na uwezo wa kusimamia matangazo na kuwahukumu waandishi habari na vyombo vya habari vitakavyo tangaza habari zisizothibitishwa na serikali au za uwongo.

Bw. Mboya anasema mswada huo unahujumu katiba ya nchi ambayo inahakikisha uhuru wa kujieleza. Anasema Shirika lake pamoja na waandishi habari na Wakenya wana wasi wasi na mswada huo.

Kufuatana na mswada huo yeyote atakae kiuka kanuni za uwandishi habari atatozwa fini ya hadi shilingi milioni 20 za Kenya sawa na dola 240,000.

No comments: