Ivory
Coast ndio inazalisha kiwango kikubwa zaidi cha Kakao duniani
Mahakama nchini Ivory Coast
imewafunga jela watu 15 waliokuwa maafisa wakuu watendaji katika sekta ya
Kahawa na Kakao nchini humo.
Maafisa hao walikuwa wanafanya kazi
katika baraza la serikali la kudhibiti mauzo ya Kakao na kahawa na kila mmoja
amefungwa jela miaka ishirini.
Maafisa wengine 15 waliachiliwa kwa
kutopatikana na hatia mjini Abidjan.
Washitakiwa wanaojulikana kama wakuu
wa biashara za Kakao, pia waliamrishwa kulipa faini ya hadi dola milioni lakini
moja na arobaini.
Wamepatikana na hatia ya kufuja
viwango vikubwa vya pesa za serikali zilizotokana na mapato ya kodi.
Maafisa hao walikamatwa mwaka 2008
baada ya aliyekuwa rais Laurent Gbagbo kuamuru uchunguzi kufanywa kutokana na
madai ya ufisadi katika sekta ya Kahawa na Kakao.
Gbagbo alishindwa katika uchaguzi wa
mwaka 2010 lakini akakataa kukubali matokeo hadi alipoondolewa mamlakani na
wanajeshi watiifu kwa rais wa sasa Alassane Ouatarra manmo mwaka 2011.
Gbagbo sasa yuko katika mahakama ya
kimataifa ya uhalifu akisubiri kuanza kwa kesi yake ambapo anatuhumiwa kwa kosa
la uhalifu dhidi ya binadamu. Gbagbo amekanusha madai hayo.
Ivory Coast ndio ndhi inayozalisha
kiwango kikubwa zaidi cha kakao , ingawa sekta hiyo imedumaa kwa miaka mingo
kutokana na mgogoro wa kisiasa wa miaka mingi nchini humo.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment