Magaidi
wlaivamia Westgate kwa siku nne na kuwashika mateka wakenya waliokuwemo ndani
ya jengo hilo wakati wa shambulizi hilo
Wanaume wanne wamefikishwa mahakamani nchini Kenya baada ya
kuhusishwa na shambulizi la kigaidi lililofanyika dhidi ya jengo la Westgate
nchini Kenya mwezi Septemba.
Wanne hao wote walikanusha mashitaka hayo ikiwemo kosa la
kuingia nchini bila vibali halali pamoja na kumiliki stakabadhi bandia za
kujitambulisha.
Mahakama imeamuru wawekwe rumande.
Kundi la kigaidi la Somalia, Al Shabaab lilikiri kufanya
shambulizi hilo la kigaidi ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.
Wanne hao walishitakiwa kwa kosa la kuhusika na shambulizi
hilo la kigaidi ingawa hakuna hata mmoja alikuwemo ndani ya Jengo la Westgate
wakati wa shambulizi hilo.
Wanne hao raia wa Somalia ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban
Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan.
Washukiwa hao ambao hawakuwa na mawakili walizuiliwa rumande
kwa wiki moja baada ya kiongozi wa mashitaka kuomba muda zaidi kufanya
uchunguzi.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment