Kiongozi
wa Taliban Pakistan Hakimullah Mehsud aliyeuawa kwa ndege isiyo na rubani
Pakistan imepinga vikali shambulio
lililomuua kiongozi wa kikundi cha Taliban cha Pakistan, Hakimullah Mehsud.
Kiongozi huyo wa Taliban nchini
Pakistan aliuawa katika shambulio la kutumia ndege isiyo na rubani.
Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Chaudry Nisar Ali Khan amesema kifo cha Hakimullah Mehsud kimeharibu jaribio la serikali ya Pakistan la kuwa na mazungumzo ya amani na wapiganaji wa Taliban.
Ujumbe wa serikali ya Pakistan
ulikuwa ukijitayarisha kukutana na wawakilishi wa Taliban katika mji wa
Waziristan, kaskazini mwa nchi hiyo.
Habari zinasema wapiganaji wa Taliban
wako katika hatua ya kumchagua mrithi wa nafasi ya Hakimullah Mehsud.
Hata hivyo bado hajatajwa ni nani.
Majeshi ya usalama yamewekwa katika
hali ya tahadhari ya hali ya juu nchini Pakistan.
Katika matukio yaliyopita, Taliban
walifanya mashambulio ya kulipiza kisasi kutokana na kuuawa kwa makamanda wake.
Hakimullah Mehsud, ameuawa kwa
kutumia ndege zisizokuwa na rubani, shambulio hilo lililenga gari alimokuwa
anasafiria Mehsud, Kaskazini Magharibi mwa Waziristan.
Hakimullah Mehsud alijulikana sana mwaka
2007 kama kamanda wa mwasisi wa kundi la Baitullah Mehsud, alipowakamata
wanajeshi 300 wa Pakistani .
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment