na Danson Kaijage, Dodoma
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne
Kilango (CCM), amewashambulia baadhi ya mawaziri wanaokaa vikaoni kupika
majungu na kuwakwamisha mawaziri na wabunge wachapaka kazi.
Kilango alitoa kauli hiyo juzi
alipokuwa akichangia mjadala wa Kamati ya Mipango ya Taifa ya mwaka 2014/16.
Kilango alisema taifa haliwezi kuwa
na maendeleo na kamwe mipango haiwezi kukamilika kama baadhi ya mawaziri na
wabunge wazembe wanakaa vikao kwa ajili ya kuwadhoofisa mawazri na wabunge
wachapa kazi.
Kilango alisema serikali imekuwa na
baadhi ya watumishi ambao kazi yao ni kupika majungu dhidi ya watumishi wachapa
kazi.
Mbunge huyo alisema Watanzania
wanatakiwa kutambua kuwa baadhi ya wanasiasa si wachapa kazi na badala yake
wanakaa bungeni kwa ajili ya kuwalaumu wengine.
Alisema inasikitisha kuona Tanzania
inakuwa na mipango mingi lakini haitekelezeki na zipo nchi nyingi ambazo
zinakuja kujifunza mipango nchini na zinafanikiwa lakini Tanzania inaendelea
kuwa maskini.
Kwa upange wake Mbunge wa Viti
Maalumu, Cecilia Pareso (CHADEMA) alisema serikali bado inashindwa kutekeleza
mipango yake kutokana na kuwa na mipango mingi ambayo haitekelezeki.
Pareso alitoa sababu nyingine ya
kushindwa kwa mpango huo kuwa ni kutokana na bajeti ya serikali kuwa tegemezi.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Felister
Bura (CCM), alisema kuwa anachoshwa na serikali kuwa na mpango wa kuhamia
Dodoma lakini mpango huo upo katika makaratasi tu.
Chanzo:
Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment