Mbunge
wa Nzegamkoani Tabora ,Dkt.Hamisi Kig wangalla ,amesema bado ana dhamira ya
kuwasi lisha hoja ya kumng’ oa madarakani Spika wa B unge, Bi.Anne Makinda.
Alisema
uvumi ulioenea kuwa hoja yake imeondolewa kwa agizo la Chama Cha Mapinduzi
(CCM), hauna ukweli.
Dkt.
Kigwangalla aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara u
lioshirikisha wakazi wa jimbo hilo na vitongoji vya ke uliofanyika katika
Uwanja wa Parking.
Katika
mkutano huo, Dkt. Kigwangalla aliulizwa swali na mkazi wa jimbo hilo kama kweli
ana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda, anayetoka na na chama chake.
“Mheshimiwa
mbunge,naomba utu thibitishie kama una uwezo wa kumng’oa Spika wa Bunge
(Makinda), kama ulivyotangaza dhamira ya kuw asilisha hoja binafsi bungeni ili
bunge liweze kumng’oa.
“Kwa
jinsi tunavyofahamu utaratibu ndan i ya CCM, huna ubavu wa kufanya hivyo , ina
onesha ulikuwa ukijifurahisha tu,”alihoji mwananchi huyo.
Mwananchi
huyo aliongeza kuwa, kwa kawaida CCM ina utaratibu wa kuzuia hatua mbalimbali
zinazotaka kuchukuliwa na wanachama wake hivyo alimshauri Dkt.Kigwangalla,
aacha ne na hoja hiyo kwani hana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda.
Akijibu
swali hilo,Dkt. Kigwangalla alisema,si kw eli kwamba CCM ina utaratibu wa
kuondoa kin yemela hoja ambazo haikubaliani nazo ambapo suala la kutaka
kumng’oa Bi. Makinda lipo ndani ya uwezo wake na kufafanua kuwa, ho ja hiyo
haijaondolewa na hivi sasa ipo katika hatua za mwisho ili iweze kufikishwa
bungeni.
“Kwa
hili la kumng’oa Spika wa Bunge,niwaele ze wazi kuwa si kweli linaweza
kunishinda... hoja imewasilishwa na Bi. Makin da atang’oka kama nikiamua
kuendelea nayo kwa sababu tayari hoja nimeiwasilisha na nimekidhi masharti
yote.
“Hivi
tunavyoongea, hoja yangu tayari imeto ka hatua ya kwanza na kukidhi vigezo
vyote sasa inaenda hatua ya pili ambayo Kamati ya Bunge y a Haki, Maadili na
Madaraka ya Bunge,itaamua hoja yangu iingizwe bungeni au isiingizwe,”alisema .
Aliongeza
kuwa,baada ya hapo utafuata mcha kato wa mwisho ambao ni hoja hiyo kufikishwa
bungeni na yeye kuiwasilisha rasmi mbele y a Bunge ili kufanyiwa uamuzi na
wabunge wote kwa kupiga kura na kama atashinda au kushind wa,hilo ni jambo
lingine.
Dkt.Kigwangalla
alisema uamuzi wa kuo ndoka au kutoondoka kwa Spika, kutategeme au amuzi wa
wabunge wenzake na kusisitiza kuwa , CCM haiwezi kuzuia hoja hiyo bila ya
kupatiwa uamuzi na wabunge wote.
Akijibu
swali ambalo lilihusiana na fedha za ushuru wa huduma zilizotolewa na Mgodi wa
Dhahabu wa Resolute, ulioko wilayani humo, Dkt. Kigwangalla alisema fedha hizo
sh.bilioni2.340,zililipwa na mgodi huo na s asa zimehifadhiwa katika akaunti
maalumu ili baadaye zitumike kama mtaji wa kuanzishia Benki ya Maendeleo ya
Wananchi wa Nzega.
“Fedha
hizi tulizipigania kwa kiasi kikubwa hadi kuandamana lakini tulifanikiwa
kuzipata, niwathibitishie zipo salama katika akaunti maalumu tuliyoianzisha ili
baadaye ziweze kuanzisha Benki yetu ya Maendeleo ambayo itaweza kutupa mikopo
ya kuendesha shughuli zetu,”alisema .
Alisema
lengo lake ni kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri ili kuwasaidia wananchi
w a Nzega kubadilisha maisha yao ambapo watu watahamasishwa kujiunga katika
ushirika au SACCOS ili waweze kupewa mikopo p ia zitatumika kununulia mitambo
ya kutengeneza barabara na uchimbaji visima vya maji.
Gazeti
moja linalotoka kila siku (si Majira), liliandika habari inayosema Dkt.
Kigwangalla anadai Bi. Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha malipo ya sh.
430,000 kama posho kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na wajumbe
wa kamati nyingine ambao malipo yao ni sh. 180,000 kwa siku.
Hoja
hiyo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Tabora Mjini, Bw.
Ismail Aden Rage (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafulila
(NCCR-Mageuzi) ambao walidai hawaoni sababu ya kumuondoa Bi. Makinda
madarakani.
Bw.
Kafulila alisema hilo ni suala la wana-CCM, kwani Bi. Makinda aking’olewa
madarakani, mtu ambaye ataziba pengo lake hawezi kutoka upinzani. Hoja hiyo ya
Dkt. Kigwangalla iliibua mjadala kwa baadhi ya wabunge na wengine kukataa
kusaini karatasi ambayo walipelekewa ili kuunga mkono.
Mbunge
wa Ludewa, mkoani Njombe, Bw. Deo Filikunjombe, alisema hoja ya Dkt.
Kigwangalla imejengwa katika msingi hafifu isiyozingatia masilahi mapana ya
nchi na mtazamo finyu.
Chanzo:
Majira
No comments:
Post a Comment