Wakuu wa Niger wamewakamata wahamiaji
zaidi ya 100 wakielekea Algeria.
Wanasema watu hao wanazuwiliwa na
polisi.
Hatua hiyo inafuatia vifo vya watu
zaidi ya 90, wakiwemo wanawake na watoto, ambao walikufa kutokana na kiu wakati
wakivuka jangwa la Sahara.
Serikali ya Niger piya imetangaza
kuwa itafunga kambi zote za wahamiaji kaskazini mwa nchi, ambazo hazitambuliwi.
Katika taarifa yake iliyosomwa kwenye
televisheni serikali pia ilisema kuwa wale wote wanaoshiriki katika biashara ya
kuwasafirisha wahamiaji kimagendo, kwa kupitia Niger Kaskazini hadi Algeria na
Libya, watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali.
Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa
Niger, Mohamed Ba-zoum, ameiambia BBC kuwa mji wa Agadez peke yake, kaskazini
mwa Niger, una wahamiaji kama elfu tano kutoka nchi mbalimbali za Afrika,
kwenye kambi zisizoruhusiwa.
Chanzo: BBCSwahili
No comments:
Post a Comment