Waziri Mkuu wa Irak Nuri al-Maliki
anakutana na Rais Barack Obama mjini Washington wakati ambapo nchi yake
inakabiliwa na wimbi kubwa la umwagikaji damu. Waziri Mkuu huyo ameenda Marekani
kuomba msaada.
Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki
Rais Obama anasifika kwa kuvimaliza
vita vya Iraq kwa kuyaondoa majeshi ya Marekani . Lakini Obama anakutana na mtu
ambae bado anapigana vita hivyo-Waziri Mkuu Nuri al -Maliki.
Waziri Mkuu al-Maliki anakutana na
Rais Obama wakati ambapo umwagikaji damu umefikia kiwango kisichokuwa na
mithili nchini Iraq tokea mwaka 2008. Waziri Mkuu wa Iraq ameomba msaada wa
Marekani ili aweze kukabiliana na hali hiyo miaka miwili baada ya majeshi ya
Marekani kuondoka. Waziri Mkuu al- Maliki ameomba msaada wa zana zaidi za
kijeshi sambamba na ushirikiano mkubwa zaidi katika mambo ya usalama baina ya
nchi yake na Marekani .
Watu takriban 1000 wameuawa
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara za
afya, mambo ya ndani na ulinzi mwezi uliopita watu takriban 1000 waliuawa
nchini Irak. Kati ya hao, 855 walikuwa raia,65 walikuwa polisi na wanajeshi 44.
Watu wengine 1600 walijeruhiwa.Lakini taarifa ya Umoja wa Mataifa inaonyesha
kwamba waliouawa ni wengi zaidi.
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa
Nickolay Mladenov amesema mauaji yanayofanyika kiholela yanaendelea mtindo
mmoja. Waziri Mkuu wa Iraq ameifafanisha hali anayopambana nayo katika nchi
yake inayotokana na mashambulio yanayofanywa na wapiganaji wenye uhusiano na
Al-Qaeda na vita vikuu vya tatu.
Miaka miwili baada ya majeshi ya
Marekani kuondoka Iraq nchi hiyo imesimama kwenye ukingo wa vita vingine vya
kimadhehebu .Mauaji yameendelea leo(ijumaa) ambapo watu wanne waliuawa
kaskazini mwa nchi hiyo.
Waziri Mkuu al-Maliki anatarajiwa
kuiomba Marekani isaidie zaidi katika juhudi za kupambana na umwagijaki damu
nchi mwake. Mwezi uliopita sehemu kadhaa za hadhara zilishambuliwa ikiwa pamoja
na mikahawa, na bustani za mapimziko.Watu waliokuwa mazikoni pia
waliwashambuliwa mara kwa.
Hata kwa Iraq mauaji yamezdi
Mtaalamu wa masuala ya Iraq kutoka
Wakfu wa Ujerumani , Friedrich-Naumann ,Falko Walde amesema Iraq haijawahi kwua
na utulivu tokea kuangushwa kwa Saddam Hussein.Ghasia zimetokea wakati wote
lakini amesema hali ya sasa ni mbaya sana. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani
imesema watu wasiopungua 6,000 wameshaua mnamo mwaka huu nchini Iraq
Maafisa wa Ikulu ya Marekani wamesema
Rais Obama atalijadili suala la usalama na Waziri Mkuu al-Maliki na kujaribu
kutafuta njia za kupunguza umwagikaji wa damu nchini Iraq.
Mwandishi:Mtullya Abdu.afp,rtre
Mhariri: Yusuf Saumu
No comments:
Post a Comment