Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu sita kwa tuhuma
za kuhusika na tukio la kumvamia, kumjeruhi vibaya kwa mapanga sehemu
mbalimbali za mwili hasa kichwani, Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt.
Sengondo Mvungi.
Dkt.Mvungi
ambaye pia ni Mjumbe wa Ha lmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, amelazwa
katika Chumba cha Wagonjwa Wana ohitaji Uangalizi Maalumu (ICU),kwenye
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akiwa ha jitambui.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Kamishna Suleiman Kova, alisema Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Novemba 3
mw aka huu, Mpigi Magohe , mpakani mwa Mkoa wa DaresSalaam na Pwani.
Alisema
katika tukio hilo watuhumiwa waliiba kompyuta mpakato moja aina ya HP,simu
mbili za mkononi pamoja na pesa taslimu sh.milioni moja.
“Baada
ya tukio polisi walianza ms ako mkali kwa kushirikiana na raia , tulifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa na baada ya kupekuliwa walikutwa na dawa za kulevya aina
ya bhangi puli 17 pamoja na gongo lita 15,”alisema.
Aliongeza
kuwa,jeshi hilo bado linaendelea n a msako ili kuwabaini watuhumiwa wengine.
James
Mbatia azungumza
Akizungumza
na waandishi wa habari hospitalini hapo,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa,
Bw.James Mbatia, alisema hali ya Dkt. Mvungi imeanza kuimarika lakini bado
hajaanza kupataf ahamu.
“Leo
hali yake inatia matumaini tofauti na alivyoletwa,kama ataendelea hivi mambo
yatakuwa mazuri zaidi,”alisema.
Aliongeza
kuwa,leo familia yake itafanya misa ya kumuombea Dkt.Mvungi ili apate nafuu
ambayo itafanyika katika Kanisa la St.Joseph , P osta Dar es Salaam, kuanzia
saa 10 jioni .
“Nawashukuru
Watanzania wote wakiwemo Mashekhe na Wanazuoni wa Kiislamu kwa kuja kumuona,
kumuombea ili aweze kupona haraka,” alisema Bw. Mbatia.
Naye
Msemaji wa Taasisi ya Mifupa(MOI ), Bw. Jumaa Almas, alisema Dkt.Mvungi anae
ndelea vizuri tofauti na alivyokuja.
“Madaktari
wanaendelea kumpa matibabu lakini hadi sasa, bado hajapata fahamu,yupo katika
chumba cha uangalizi maalumu alisema Bw. Almas
No comments:
Post a Comment