Lambert
Mende Msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo imesema majeshi yake kwa kushirikiana na kile kikosi maalum cha Umoja
wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi wa M23 kimewapiga waasi hao
katika ngome yao ya mwisho.
Msemaji wa Serikali Lambert Mende
ameiambia BBC kuwa wapigani waliobaki wa M23 wanaweza wakawa wamekimbia ,
wamevuka mpaka au wamejisalimisha.
Mende amesema kikosi maalum cha
majeshi ya nchi hiyo kimeharibu silaha za waasi hao usiku kucha na inasadikiwa
kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo la M23 Sultani Makenga ni miongoni mwa
waliovuka mpaka na kuingia Rwanda au Uganda.
Wakati huo huo viongozi wa nchi za
SADC wanaokutana nchini Afrika Kusini wamezunguzia mgogoro wa Jumuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo na kuwataka viongozi kundi la waasi wa M23 kutangaza
kusimamisha mapigano.
Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano
huo imesema kama waasi hao watachukua hatua hiyo mkataba wa amani unaweza
kusainiwa ndani siku tano zijazo.
Chanzo:
BBCSwahili
No comments:
Post a Comment