Shangazi wa Rais Uhuru Kenyatta
amekuwa moja wapo wa waathiriwa wa wizi wa magari kwa kutumia nguvu nchini
Kenya, baada ya kushambuliwa na kuibiwa gari lake akiwa katika msongamano wa
magari kwenye njia kuu ya Uhuru.
Watu watatu walokuwa na bunduki
walingia kwa nguvu ndani ya gari la Bi. Njeri Muhoho, mwenye umri wa miaka 56,
na kumzungusha katika jiji la Nairobi kwa karibu saa mbili kabla ya kumshusha
karibu na shule moja ya kimataifa katika mtaa wa kaskazini wa Gigiri.
Bi. Muhoho, ambae ni mke wa mkuu wa zaamani
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya, George Muhoho, aliwambia polisi
kwamba alikua garini pamoja na mwanamume mwenye umri wa miaka 25 wakati gengi
la watu watatu walipowashambulia Jumanne, saa mbili na nusu usiku.
Polisi wanaeleza kwamba walishambuliwa
wakiwa wanasubiri taa ya kuongoza magari kubadilika kuwa kijani, na aliibiwa Sh
20,000 za Kenya, pamoja na kadi yake ya benki ATM, na leseni ya kuendesha gari.
Mkuu wa polisi mjini Nairobi Benson
Kibue anasema baada ya kuwashusha, wezi hao watatu walelekea mahala
isipojulikana na gari lao la aina ya Nissan. Msako unafanyika kutafuta gengi la
watu hao.
Chanzo: VOA Swahili
No comments:
Post a Comment