Serikali ya Tanzania imesema kuwa
imebaini kuwepo kwa biashara haramu ya kusafirisha watoto wa kike kwenda nchini
China kwa lengo la kuwashirikisha katika ukahaba ambao unadaiwa kusababisha
kunyanyaswa kwa wasichana hao na wengine kuuawa.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano
wa kimatifa nchini humo Bernard Membe amesema serikali itatuma wachunguzi
nchini Uchina kuchunguza biashara hiyo. Hatua hiyo imechukuliwa mwezi mmoja
baada ya msichana mmoja Mtanzania kuuawa kikatili katika mji wa Guangzhou
nchini Uchina.
Waziri Membe amesema huenda baadhi ya
wahusika wa bishara hiyo ni Watanzania wanaosafirisha wasichana wa dogo kwa
kisingizio cha kuwatafutia ajira. Baadhi ya wanaosafirishwa hujipata pabaya
baada ya kuwasili Uchina ambapo hunyang'anywa hati zao za usafiri na kulazimishwa
kushiriki ukahaba. Baadhi ya wakaazi wa Dar es laam waliozungumza na BBC
wameelezea kusikitishwa na vitendo hivyo na kuitaka serikali ichukue hatua.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment