Kamba inayotumika kunyongea
Shirika la Amnesty International limetoa ripoti inayosema idadi ya watu waliopewa adhabu ya kifo na kunyongwa imeongezeka duniani. Ripoti hiyo inasema watu 778 walinyongwa mwaka jana katika nchi 22.
Je ni kosa gani linaloweza
kusababisha mtu ahukumiwe adhabu ya kifo kati ya haya yafuatayo rushwa,
uzinifu, biasharaya mihadarati, wizi wa gari au kutazama tamthilia iliyopigwa
marufuku? Jibu ni kwamba kila kosa kati ya hayo linaweza kusababisha mtu apewe
adhabu ya kifo. Swali hilo limepelekwa katika mtandao wa internet na Shirika la
kutetea haki za binadamu, Amnesty International ikiwa ni kiini cha ujumbe wa
ripoti yake ya mwaka 2014 inayoitwa "Adhabu ya Kifo" Ujumbe unasema
adhabu ya juu kabisa ambayo mtu anaweza kuifikiria haitolewi kwa kosa la mauaji
tu.
Kile ambacho katika nchi fulani
kinazingatiwa kuwa ni kosa la mauaji kinategemea na utamaduni, dini na hali ya
kisiasa ya nchi hiyo-Lakini pia hutegemea na jinsi wenye madaraka wanavyoamua! Mfano
juu ya mtu kupewa adhabu ya kifo kwa sababu tu ya kutazama tamthilia, unatoka
Korea ya Kaskazini. Hakuna mengi juu ya Korea ya kaskazini katika ripoti
iliyotolewa mnamo mwaka huu ya Shirika la Kutetea haki za binadamu, Amnesty
International.
Watu wanaendelea kunyongwa nchini
humo.Huo ni ukweli.Lakini shirika la Amnesty international halina taarifa
zinazoweza kuitia hatiani Korea ya Kaskazini
Hali ya adhabu ya kifo ilivyo Korea
Kaskazini
Msemaji wa shirika hilo Ferdinand
Muggenthaler ameeleza katika mahajiano na DW kwamba, ni vigumu kuhusu Korea ya
Kaskazini kusema iwapo mtu ananyongwa kutokana na hukumu ya mahakama, au ni
mauaji yanayofanywa na serikali au mtu anapotea tu.!
Kwa jumla shirika la Kutetea haki za
binadamu la Amnesty International huchapisha zile takwimu katika ripoti zake za
mwaka ambazo hutokana ama na vyanzo rasmi au idadi zilizothibitishwa kutokana
na uchunguzi au kutokana na taarifa za jamaa wa walionyongwa.
Kitanda kinachotumika katika adhabu ya kifo
Hakuna nchi inayojifungia ndani kama
Korea ya Kaskazini. Lakini pia zipo nchi nyingine ambazo hazitoi taarifa juu ya
adhabu za kifo zinazotolewa au juu ya hukumu za kifo zinazotekelezwa. Mfano ni
China. Kwa mujibu wa duru za kuaminika, maalfu ya watu wananyongwa nchini humo
lakini habari juu ya watu hao zinafichwa na kwa hivyo idadi halisi haijulikani.
Ripoti ya Shirika la kutetea haki za
binadamu Amnesty International inasema ongezeko la idadi ya watu walionyongwa
mwaka jana duniani imetokana na adhabu za kifo zilizotekelezwa nchini Iran,
Iraq na Saudi Arabia.
Marekani pia ni miongoni mwa nchi
tano duniani ambako idadi kubwa ya watu walinyongwa. Shirika hilo pia limearifu
hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2013 watu 23,000 duniani kote, bado walikuwa
wanasubiri kunyongwa.
Mwandishi:Gessat,Michael
Tafsiri:Mtullya Abdu.
Mhariri: Gakuba Daniel
No comments:
Post a Comment