Rais Obama akitoa taarifa rasmi baada ya unyakuzi wa Crimea
Mzozo kuhusu Crimea na Ukraine utajadiliwa leo na viongozi wa
mataifa mbalimbali akiwemo rais Obama.
Viongozi hao wamejumuika katika kongamano la kujadili usalama
wa nyuklia lakini ajenda hio inatarajiwa kugubikwa na mazungumzo kuhusu hatua
ya Urusi kunyakua eneo la Crimea. Rais wa Urusi Vladmir Putin amesusia mkutano
huo na kumtuma waziri wake wa maswala ya kigeni.
Rais Obama,Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na viongozi
wenzao kutoka mataifa saba yaliyoendelea zaidi watakutana katika kikao maalum
kuzungumzia hatua zaidi za kuiadhibu Urusi.
Huenda Moscow ikatengwa zaidi katika maswala ya kisiasa na
kiuchumi.Tayari mataifa ya Ulaya yameapa kuiwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment