Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo amefungua hospitali mjini Kinshasa miaka 60 tangu hospitali
hiyo kuanza kujengwa.
Waziri wa Afya, Felix Kabange Numbi,
alisema hiyo ndio hospitali yenye vifaa vya kisasa kabisa nchini humo.
Ilianza kujengwa mwaka wa 1954 lakini
ujenzi ukasimama wakati wa uhuru mwaka wa 1960 na kuanza tena miaka mingi
baadae.
Hospitali hiyo hatimae ilimalizwa na
Uchina miaka mitatu iliyopita lakini haikuweza kufunguliwa kwa sababu ya uhaba
wa vifaa na wafanyakazi wenye ujuzi.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment