ZAIDI ya watu 64,000 nchini huugua
Kifua Kikuu (TB) kila mwaka sawa na wastani wa wagonjwa 176 kwa siku.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es
Salaam jana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu na
Ukimwi Temeke, Joseph Mapunda, katika maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu
Duniani
Alisema takwimu hizo zimepatikana kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia mpango wa taifa wa
kudhibiti kifua kikuu na ukoma.
Alisema idadi kubwa ya watu
wanaoambukizwa ugonjwa huo ni watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU), walio
katika msongamano na wazee wenye zaidi ya miaka 60.
Alitaja makundi mengine ambayo wapo
katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo ni watoto chini ya miaka mitano, watu
wenye lishe duni na wenye magonjwa ya muda mrefu kama kisukari na saratani.
“Kuna idadi kubwa ya wagonjwa
wanaopatikana vijijini lakini kutokana na ukosefu wa fedha na serikali kutotoa
kipaumbele katika hili, ugonjwa huu umekuwa chanzo cha kupoteza nguvu kazi ya
taifa kila kukicha” alisema.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Hewa
katika Hospitali ya Aga Khan, Dk. Naeem Sultan, alisema kama watu wakiwa na
utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara kutokomea magonjwa ya hewa ni suala
linalowezekana.
No comments:
Post a Comment