Wanasayansi nchini Ufaransa wamebaini
kwamba virusi vya Ugonjwa wa Ebola ndio chanzo cha ugonjwa wa homa ya
haemorajic nchini Guinea ambayo inaaminika kuwauwa karibia watu sitini.
Ugonjwa huo ambao unaweza kuambukizwa
kwa haraka ulianza nchini humo yapata majuma sita yaliopita.
Dalili za ugonjwa huo ni kutoka
damu,kuharisha pamoja na kutapika.
Afisa mmoja wa wizara ya afya nchini
Guinea amesema kuwa takriban visa vinane vya ugonjwa huo vimeripotiwa hususan
kusini mwa taifa hilo.
Amsema kuwa serikali ya taifa hilo
inatumia kila njia kukabiliana na ugonjwa huo lakini inaendelea kushindwa.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa
wa Ebola ambao husambazwa kupitia kugusana na walioambukizwa.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment