Kiongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood Mohamed Badie.
Kesi dhidi ya wafuasi 700 wa
aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi, imeanza kusikilizwa mjini Cairo.
Miasaba hao ambao pia ni wafuasi wa
chama kilichopigwa marufuku cha Muslim Brotherhhood, wanakabiliwa na tuhuma za
kufanya maandamano yaliyozua ghasia mwaka jana.
Miongoni mwa watuhumiwa ni kiongozi
wa vuguvugu hilo, Mohamed Badie.
Maafisa wa utawala wanaseama kuwa
Badie hatafikishwa mahakamani leo kutokana na sababu za kiusalama.
Kesi hiyo inaendeshwa bila ya
watuhumiwa wengi kupo mahakamani.
Ni watu 60 pekee waliokuwa mahakamani
siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watuhumiwa wengine miatano walihukumiwa kifo.
Wengi Nchini Misri wamelaani hukumu
hiyo.
Walihukumiwa baada ya kupatikana na
hatia kwa mashitaka kadhaa ikiwemo kumuua afisa wa polisi baada ya kuzuka
ghasia mnamo Agosti katika makabiliano na maafisa wa usalama, wakipinga
kupinduliwa kwa Mohammed Morsi.
Mawakili wao wanasema hawakuwa na
nafasi ya kujitetea.
No comments:
Post a Comment