Manchester United imepangwa kucheza
na Bayern Munich katika michuano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani
Ulaya huku Chelsea ikipangwa kukutana na Paris St-Germain.
Mabingwa wa ligi ya Uhispania,
Barcelona watapambana na Atletico Madrid, huku Real Madrid ikipangwa kukutana
na Borussia Dortmund.
Mechi zao za mzunguko wa kwanza
zitaanza tarehe 1 mpaka 2 mwezi Aprili na marudiano yatakuwa tarehe 8-9 Aprili.
Fainali ya michuano hiyo itachezwa
katika uwanja jijini Lisbon wa Estadio da Luz tarehe 24 mwezi Mei.
Manchester na Bayern wanakutana tena
tangu mwaka 1999 kwenye fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ambapo Ole
Gunnar Solkjaer na Teddy Sheringham waliiwezesha Manchester kutwaa kikombe
chini ya Kocha wao Alex Ferguson.
Mara baada ya kupangwa kwa timu hizo
nchini Switzerland, kiungo mshambuliaji wa Bayern, Philipp Lahm amesema kuwa
hawawezi kutetereshwa na nafasi waliyonayo United kwa sasa katika ligi kuu na
kusema kuwa watasafiri mpaka Manchester kwa kazi moja tu, nayo ni kufunga
magoli.
Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa
ligi itaifuata PSG nchini Ufaransa katika mzunguko wa kwanza.
Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment