Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama Marekani na Ulaya
Rais Obama yuko mjini Brussels ambapo
atakutana na viongozi wa muungano wa Ulaya na shirika la kujihami la NATO,
kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Kwenye hotuba muhimu kuhusu sera Rais
Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama wa Marekani na nchi za Ulaya na
pia kuonya Urusi dhidi ya kukiuka sheria za kimataifa.
Akizungumza mjini the Hague kabla ya
kuelekea Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya Urusi kutwaa eneo la Crimea
kutoka kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.
Hatahivyo amesema bado kuna nafasi ya
Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo
zaidi vya kiuchumi. Amesema japo huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa
dunia,Urusi ndio itakayoathirika zaidi.
Mkutano huo pia unatarajiwa
kuzingatia maswala ya kibiashara na pia wasiwasi kwamba Marekani imekuwa
ikichunguza kisiri shuguli za washirika wake kutoka nchi za Ulaya.
No comments:
Post a Comment