Waziri wa ulinzi wa misri na mkuu wa
jeshi Abdel Fatahh al-Sissi ametangaza katika hotuba kwa taifa kupitia
televisheni Jumatano kwamba anajiuzulu kutoka wadhifa wake wa
waziri wa ulinzi na kugombania kiti cha rais katika uchaguzi ujao unaotarajiwa
kufanyika mwezi ujao. Tangazo hilo linafikisha kikomo
Field Marshal Sissi anasema
anajiuzulu kama waziri wa ulinzi na anagombania kiti cha rais katika tangazo
kwenye kwenye televisheni ya taifa, baada ya kukutana na baraza kuu la
majeshi ya taifa akiwemo kaimu rais Adly
Mansour.
Anasema kwamba anajitokeza kwa mara
ya mwisho katika mavazi ya kijeshi baada ya miaka 45 ya kulihudumia taifa, lakini
anasema ataendelea kulilinda taifa katika jukumu jipya. Alisema hakuna
anayeweza kuwa rais dhidi ya matakwa ya wananchi na bila ya uungaji mkono wao,
kama ilivyokua enzi za zamani.
Tangazo hilo halikuwashangaza wengi
kwani kulikuwepo na uvumi wa wiki kadhaa
kwamba Jenerali Sissi atagombania kiti cha rais. Katika hotuba yake alitoa wito
kwa wamisri kumuunga mkono katika juhudi zake kugombania nafasi kuu hiyo ya
taifa.
Jenerali alisema wamisri wanahaki ya
kuishi kwa hadhi na uhuru lakini ni lazima kila mtu afanye kazi na kuzalisha
matunda kuiweka Misri katika nafasi yake inayostahiki miongoni mwa mataifa
yenye ustaarabu. Vile vile alisema Misri
ni taifa wa wakazi wake wote na hakuna yeyote anayebidi kutengwa.
Tangazo lilitolewa kukiwepo na
mapambano ya hapa na pale kati ya polisi na wanafunzi wanaounga mkono kundi
lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood katika chuo kikuu cha Cairo na
maeneo mengine kadhaa ya mji mkuu huo.
Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi wakazi wa jioni na kuna ripoti
za watu kadhaa waliojeruhiwa.
Wafuasi wa Jenerali Sissi walikusanyika katika maeneo kadhaa ya mji
mkuu wakati fashasha zilifyatuliwa kwa kutarajia kutangazwa kwamba anagombania
kiti cha rais.
Baraza la mawaziri la Misri
linatarajiwa kukutana Alhamisi asubuhi
kumteuwa mtu atakaye chukua nafasi ya Jenerali. Vituo vya televisheni za
setalaiti vya kiarabu vimeripoti kwamba Jenerali mkongwe Sobhi Sudqi
amepandishwa cheo na atachukua nafasi ya Jenerali Sissi.
Waziri mkuu Ibrahim Mehleb amesema
serikali yake itabaki na msimamo wa kutopendelea upande wowote katika utaratibu wa uchaguzi.
Kundi la Muslim brother hood katika
ukurasa wake wa tovuti kwamba kujitangaza mgombea kiti cha rais kunamaanisha
Jenerali Sissi alipanga njama ya kumpindua rais Mohamed Morsi .
No comments:
Post a Comment