Rais Bouteflika
Maelfu ya raia wa upinzani nchini
Algeria wamehudhuria mkutano mkubwa wa hadhara katika mji mkuu wa Algiers ili
kutaka watu wasusie uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi ujao.
Vyama vya upinzani vikiwemo vile vya
dini vimepinga harakati za rais Abdelaziz Bouteflika kutaka kuliongoza taifa
hilo kwa muhula mwingine wa miaka minne.
Wanasema kuwa hafai kuliongoza taifa
hilo baada ya ugonjwa wa kupooza kumuathiri vibaya mwaka uliopita.
Maandamano kumpinga Rais Bouteflika
Mkutano huo ulifanyika ndani ya
ukumbi wa michezo ambapo watu 5000 walikusanyika wakilaani harakati za
Bouteflika kutaka kugombea urais kwa muhula wa nne.
Wanataka mageuzi ya sheria pamoja na
kuishinikiza serikali kuangamiza ufisadi.
Bwana Bouteflika ambaye ana umri wa
miaka 77 amekuwa haonekani hadharani miezi ya hivi karibuni,lakini waandishi
wanasema kuwa ushawishi alionao katika chama tawala, jeshi na miongoni mwa
wafanyibiashara huenda ukamsaidia kuchaguliwa kwa muhula mwingine.
Amekuwa mamlakani tangu mwaka 1999 na
alifutilia mbali sheria za katiba mwaka 2008 ambazo zilimruhusu tu kuwa
mamlakani kwa mihula miwili.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment