Al Shabaab
Mamia ya wanajeshi wa Muungano wa
Afrika wanaukaribia mji muhimu wa Koryoley, ulio umbali wa kilomita 90 Kusini
Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya
udhibiti wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab kwa miaka mitano iliyopita.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo
hilo anasema kuwa wanajeshi hao wako umbali wa kilomita 10 kutoka mjini humo.
Anasema kuwa ikiwa wanajeshi hao
wataukomba mji huo, utakuwa ukombozi wao mkubwa wa mji tangu kuanza harakati
hizo dhidi ya Al Shabaab mwezi Machi mwaka jana wakiungwa mkono na Umoja wa
Mataifa.
Wanajeshi hao wamefanikiwa kukomboa
miji mingine muhimu na hata kuwatimua wapiganaji hao kutoka katika ngome zao
kubwa.
Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka Uganda,
wakisaidiwa na wanajeshi wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia pamoja na wanajeshi
wa Somalia.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment