Familia za abiria wa ndege
iliyotoweka ya Malaysia majuma mawili yaliyopita, wamekabiliana na polisi nje
ya ubalozi wa Malaysia mjini Beijing.
Wakiwa wamejawa na ghadhabu,
wamelitaka shirika la ndege ya taifa hilo mjini Kuala Lumpur kueleza
kilIchofanyika.
Jamaa hao walibeba mabango yenye
maandishi "Save MH370" jamaa hao wenye hasira walikabiliana na polisi
na kuwalemea hadi kuingia katika ofisi ya ubalozi huo.
Walifoka wakisema ..''Tunataka
ukweli." hii ni ishara ya hasira na mafadhaiko wanayopitIa jamaa hao wa
watu waliopotea.
Kero la jamaa hao limekuja baada ya
waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak kusema udadisi wa data ya Satelite
ulionyesha kuwa safari ya ndege hiyo iliishia baharini Kusini mwa Australia.
Serikali ya China imeomba kuona data
hiyo ambayo Malaysia imeamini kiasi cha kutoa msimamo wake.
Shughulii ya kuitafuta ndege hiyo
MH370 imesitishwa kutokana na mawimbi makali baharini.
Mataifa mbali mbali yalijitolea
kusaidia Malaysia kuitafuta nmdege hiyo, juhudi ambazo zililengwa zaidi katika
bahari ya Kusini Magharibi mwa mji wa Australia Perth
Ndege hiyo MH370 ilipotea tarehe nane
mwezi Machi, ilipokuwa njiani kuelekea Beijing kutoka Kuala Lumpur.
Ilikuwa imebeba abiria 239 ikiwemo
raia 153 wa China.
Maandamano ya umma ni haramu nchini
China,lakini hadi kufikia watu hawa wakapanga maandamano kama hayo ni ishara
kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini kabisa.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment